
Sendiga akemea watoto kunyimwa fursa ya elimu
Simanjiro. Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amekemea kitendo cha wazazi na walezi wanaowazuia watoto wao wa kiume kwenda shule, badala yake kuwageuza wachungaji wa mifugo. Amesema nyakati hizi si za wazazi kupuuzia elimu kwa watoto wao badala yake wawe mstari wa mbele kuwahimiza kuipenda. Sendiga amesema hata watoto wa kike nao wananyimwa fursa…