DKT. NCHEMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI WA ECOBANK

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania, Bw. Charles Asiedu, baada ya kikao kilichoangazia ushirikiano kati ya Serikali na benki hiyo, jijini Dodoma. Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania, Bw. Charles Asiedu, kuhusu ushirikiano kati ya…

Read More

Tanga Uwasa yafungua njia matumizi ya hatifungani

Dodoma. Serikali imezitaka taasisi zake kutumia utaratibu wa hatifungani kugharimia miradi ya maendeleo badala ya kutegemea bajeti pekee. Agizo hilo limetolewa baada ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa) kuorodhesha hatifungani ya miundombinu ya maji na utunzaji wa mazingira Mkoa wa Tanga katika Soko la Hisa la Dar es Salaam. Uorodheshwaji…

Read More

India, Pura wajadiliana sekta ya mafuta na gesi asilia

Dar es Salaam. Ubalozi wa India nchini umekutana kwa mazungumzo na Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (Pura) kupata taarifa kuhusu vitalu vya utafutaji mafuta na gesi asilia. Mazungumzo hayo yamefanyika jana Mei 15, 2024 katika ofisi za Pura na kuhudhuriwa na Katibu wa Pili wa Balozi wa India nchini Tanzania (Masuala ya…

Read More

Mkanganyiko wa takwimu, mauzo ya ufuta yakipaa

Dar es Salaam. Wakati bajeti ya Wizara ya Kilimo ya mwaka 2024/25, ikionyesha kuwa mauzo ya zao la ufuta yalifikia zaidi ya Sh1.25 trilioni kwa kipindi cha mwaka 2022/23, taarifa ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) inaonesha mauzo yalikuwa Sh715.6 bilioni kwa mwaka 2023. Licha ya kuwa takwimu hizo ni za vipindi tofauti…

Read More

Aliyeshtakiwa kwa kula, kulala Hoteli ya Serena bila kulipa afutiwa kesi

Dar es Salaam. Mahakama ya Mwanzo Kariakoo imemfutia kesi na kumwachia huru mfanyabiashara aliyeshtakiwa kwa kujipatia huduma ya chakula na malazi katika Hoteli ya Serena kwa njia ya udanganyifu. Mshtakiwa Denis Mfumbulwa (44) alidaiwa kujipatia huduma hizo zenye thamani ya Sh21.4 milioni bila kulipa, akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria. Mfumbulwa amefutiwa kesi Mahakama ikieleza…

Read More

Biashara ya mkaa pasua kichwa, yafikia Sh69.9 bilioni

Wakati dunia ikiendelea kupigia chapuo matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa ajili ya kulinda mazingira, hali bado ni tete kwa upande wa Tanzania, ambayo uuzaji wa mkaa umeongezeka kwa karibia mara 20 zaidi ndani ya mwaka mmoja. Tanzania imekuwa kinara wa kampeni ya matumizi ya nishati safi ya kupikia barani Afrika. Mara kadhaa Rais…

Read More

Bajeti ya uchaguzi, kulinda haki za raia

Dodoma. Nyongeza ya fedha kwenye bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani, imelenga kuwezesha utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai. Pia bajeti hiyo imelenga kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuliwezesha Jeshi la Polisi kutimiza majukumu yake, ikiwemo la uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani. Maombi ya…

Read More

Hali ya utulivu imeanza kurejea Kharkiv – DW – 16.05.2024

Zelensky amesema aliyevamia mkoa huo wa Kharkiv ataangamizwa kwa namna yoyote na kwa kutumia rasilimali zilizopo, huku akisifu ufanisi wa vikosi vyake na kusisitiza kuwa wanaendeleza pia mapambano katika mji wa Kupyansk, katika mkoa wa Donetsk na pia katika mji wa Vovchansk karibu na mpaka wa Urusi. Rais Zelensky ambaye amelazimika kuahirisha safari zake zote…

Read More

Apandishwa kizimbani akidaiwa kumbaka mtoto wa miaka 17

Geita. Mkazi wa Mgusu Mjini Geita Magongo Kulwa (30) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Geita akidaiwa kumbaka mtoto wa miaka 17.  Mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo, Nyakato Bigirwa, Mwendesha mashtaka Luciana Shaban amesema mshtakiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 4, 2024 huko Mgusu. Hata hivyo, mshtakiwa huyo alikana kutenda kosa hilo na…

Read More