
Hati chafu zatawala vyama vya ushirika Mara, RC aagiza Takukuru kuchunguza
Musoma. Asilimia 89 ya vyama vya ushirika mkoani Mara vilivyokaguliwa na Shirika la Usimamizi na Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika (Coasco), vimebainika kuwa na hati zisizoridhisha katika kipindi cha mwaka 2022/23. Kufuatia hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Evans Mtambi ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani humo kuanza uchunguzi mara moja….