
Ukweli kuhusu ‘ardhi inayotembea’ Muleba, athari zake kwa wananchi
Muleba. Wakati mvua katika maeneo mbalimbali nchini zikisababisha mafuriko, baadhi ya maeneo yameshuhudia maporomoko ya tope linalotembea kama maji, jambo ambalo limewastaabisha watu ambao hawakuwahi kushuhudia jambo hilo. Hicho ndiyo kinachotokea katika Kitongoji cha Kabumbilo kilichopo katika Wilaya ya Muleba mkoani Kagera, ambapo tope linalotembea kuelekea mwambao wa Ziwa Victoria, limeibua gumzo mitandaoni huku watu…