BIL 1.1 ZA TANROADS ZAREJESHA MAWASILIANO YA BARABARA NA MADARAJA YALIYOSOMBWA NA MVUA ZA EL-NINO – KATAVI

Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoani Katavi imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kufanya kazi ya matengenezo na kurejesha miundombinu ya barabara na madaraja yaliyosombwa na maji ya mafuriko ya mvua kubwa za El-nino zilizonyesha kwa wingi mkoani humo tarehe 14 na 15 Aprili 2024. Meneja wa TANROADS Mkoa wa Katavi Martin A. Mwakabende amesema…

Read More

ULEGA: TUMEJIPANGA KUIMARISHA BIASHARA YA MAZAO YA MIFUGO

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amesema wizara yake imejipanga kuyasimamia vyema mazao ya mifugo hususan maziwa, nyama na ngozi ili yazalishwe kwa ubora na kushamirisha biashara kwa lengo la kuyafanya mazao hayo kuwa na mchango mkubwa zaidi kwenye pato la Taifa. Ameyasema hayo wakati akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Nyama na…

Read More

Mafyatu wanataka muungano si mgongano

Juzi Tunda Lishe alilikoroga. Si alihoji mantiki ya Zenj kuua Tanganyika hata kutaka wadanganyika wawe na pasipoti kuingia Zenj. Baada ya kukinukisha, si kiliuma. Machawa na mazwazwa wajikombao wapate shibe si walilidhalilisha hata Bungo! Alianza mmoja aliyetaka eti Wadanganyika waingie Zenj kwa pasi ilhali Wazenj waingie bwerere na kuishi watakavyo. Tunda alihoji mantiki ya Wazenj…

Read More

Kwa nini mhimili wa nne unahitaji kuwezeshwa?

Wiki hii nzima, nimekuwa jijini Dodoma kuhudhuria mikutano mitatu muhimu ya mambo ya habari. Tulianza na mkutano mkuu wa 13 wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dotto Biteko. Ukaja mkutano wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu mstaafu, Jaji…

Read More

Mashambulizi ya Lissu alianzia Kaskazini na Rais Samia, akaigeukia Kusini 

Ndani ya wiki mbili zilizopita, Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tanzania Bara, ametoa kauli mbili nzito. Mosi, mkoani Manyara, alitamka maneno yaliyotafsiriwa kama shambulizi kwa CCM na Rais Samia Suluhu Hassan. Ya pili, aliitoa Iringa, akikituhumu chama chake kwa rushwa. Manyara, Kaskazini ya Tanzania, Lissu alizungumza kauli tata kuhusu Muungano. Kwamba Samia Mzanzibari, asingekuwa Rais wa…

Read More

Shekilango alivyofariki katikati ya misheni maalumu Uganda

Dar es Saalam. Miaka 44 imetimia tangu kufariki kwa kiongozi Mtanzania, Hussein Shekilango ambaye barabara maarufu ya Shekilango ilipewa jina hilo kwa heshima yake. Ilikuwa Jumapili ya Mei 11, 1980, Tanzania ilipompoteza waziri wake, Shekilango katika ajali ya ndege iliyotokea Arusha. Shekilango alikuwa Meneja Mkuu wa Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC) kabla ya kuchaguliwa…

Read More

RC MAKONDA TAYARI KUWAFUTA MACHOZI WAKAZI WA ARUSHA.

Hakuna hadithi nyingine zaidi ya Wewe kupata haki yako, Muhimu Njoo na Nyaraka zako zote na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda yupo tayari kukuhudumia na kupambana kwaajili yako dhidi ya wanaozuia haki yako kwa muda mrefu. Mkuu wa Mkoa Mhe. Paul Christian Makonda anakualika na kukusihi usiwe mnyonge kwasababu haki yao…

Read More