
Atolewa uvimbe wa kilo tano tumboni alioishi nao miaka 10
Geita. “Nimezaa watoto 11 lakini mtoto wangu wa mwisho niliyemzaa mwaka 2010 nilikuwa nipoteze maisha, maana nilitokwa na damu nyingi sana, nikazimia mara tatu na wakati wote wa mimba damu ilikuwa inavuja, sikujua tatizo.” Haya ni maneno ya Eveline Paulo, mkazi wa Biharamulo mkoani Kagera aliyetolewa uvimbe wenye uzito wa kilo tano tumboni. Uvimbe huo…