CCM Simiyu yakemea wajawazito kudaiwa fedha huduma za afya

Na Samwel Mwanga, Itilima MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohammed amehaidi kulivalia njuga suala la baadhi ya wahudumu wa Afya katika Wilaya ya Itilima mkoani humo wanaodaiwa kuwatoza fedha wanawake wajawazito ili waweze kupata kadi ya mahudhurio yao ya kiliniki. Pia, amesema Sera ya Taifa ya Afya inataka huduma za afya…

Read More

Profesa Mkenda awakingia kifua wanaume Rombo kwa ulevi

Dar es Salaam. Mwaka 2015 iliripotiwa wanawake wilayani Rombo kulalamika kwenda nchi jirani ya Kenya kukodi wanaume kupata unyumba, baada ya waume wao kuishiwa nguvu kwa sababu ya ulevi uliopindukia. Taarifa hiyo ilitangazwa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Lembris Mchome. Mwananchi  mwaka 2023 liliripoti habari kuwa wanaume wanaoishi pembezoni mwa Mto Mlembea, wilayani Rombo…

Read More

DKT. BITEKO ASISITIZA UMUHIMU WA ELIMU USALAMA MAHALI PA KAZI

*📌Aipongeza OSHA kuboresha utendaji* *📌Asema ufasinisi sio kuwindana, kutozana faini* *📌Ahimiza hifadi ya mazingira kukabili mabadiliko ya tabia nchi* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko mewataka waajiri kwa kushirikiana na wadau wanaendelea kuboresha mazingira ya kazi ili kuongeza usalama mahala pa kazi na kuwawezesha watumishi kufanya kazi katika mazingira rafiki…

Read More

Sababu chanjo ya HPV kupewa wasichana wadogo

Dar es Salaam. Wizara ya Afya imesema hadi kufikia jana, Aprili 27 wasichana zaidi ya milioni 4 wenye umri wa miaka 9 hadi 14 wamechanjwa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi ( ‘HPV Vaccine’) Tanzania bara na visiwani. Chanjo hiyo iliyotarajiwa kuwafikia wasichana 5,028,357 waliopo katika mikoa 31 na halmashauri 195 Tanzania bara…

Read More

NGORONGORO YAZINDUA ZOEZI LA UPIGAJI KURA KUWANIA TUZO YA KIVUTIO BORA CHA UTALII BARANI AFRIKA.

 Na Mwandishi wetu, Arusha. Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imezindua zoezi  la upigaji kura kuwania tuzo ya kivutio bora cha utalii barani Afrika kwa mwaka 2024 katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Jengo la Ngorongoro Jijini Arusha. Akizindua kampeni hiyo ya upigaji kura kaimu kamishna wa Uhifadhi NCAA Victoria Shayo amesema zoezi hilo litachukua siku…

Read More

Mwanafunzi ajinyonga baada ya mpenzi wake kukamatwa

Mufindi. Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Mgololo iliyopo katika kata ya Makungu, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, Rahel Nyasi amekutwa amejinyonga katika mti wa shamba lililopo karibu na nyumba yao. Akizungumza kwa njia ya simu leo April 28, 2024, Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Mabaoni, Zephania Masanja, amethibitisha kutokea kwa…

Read More

Serikali kununua helikopta maalumu kutafiti madini

Geita. Waziri wa Madini, Antony Mavunde amesema Serikali kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), kwa mwaka ujao wa fedha inakusudia kununua helikopta itakayofungwa vifaa maalumu vyenye uwezo wa kwenda chini umbali wa kilomita moja na kutafiti kwa kina kiwango cha madini kilichopo ardhini. Pia, Serikali inalenga kujenga maabara kubwa na ya…

Read More

Mtanzania kusaka rekodi kisiwa cha Greenland

Moshi. Kijana mmoja mkazi wa Moshi mkoani Kilimanjaro, Wilfredy Moshi anayekwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Denmark kwenye mashindao ya kutembea na kuteleza kwenye barafu katika kisiwa cha Greenland, huenda akawa Mtanzania na Mwafrika wa kwanza kufika katika kisiwa hicho. Asilimia 80 ya kisiwa cha Greenland ambacho ni kikubwa zaidi duniani na chenye watu 56,000, imefunikwa na…

Read More