Sh800 bilioni zitakavyomaliza tatizo la umeme Zanzibar

Unguja. Huenda mwarobaini wa kata, washa ya umeme, ikapatikana baada ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kuwekeza Sh800 bilioni katika miundombinu hiyo. Zanzibar inapokea umeme kupitia waya za baharini kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco). Kwa upande wa Unguja, zipo waya mbili, moja ya megawati 45 iliyowekwa mwaka 1980 na imeshatumika hadi kufikia asilimia…

Read More

Kituo cha taarifa mwarobaini kero za wananchi Mbarali

Mbarali. Wananchi wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wameeleza matumaini yao baada ya Serikali kufungua Kituo cha Taarifa (Call centre), wakisema kitawasaidia kupunguza gharama za kusafiri umbali mrefu kuwasilisha kero na kupata ufumbuzi. Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti leo Jumamosi, Machi 7, 2026, katika Kata ya Igurusi, wamesema ujio wa mfumo huo utasaidia kuokoa muda…

Read More

Vijana 308 wapewa Sh7 bilioni kutekeleza miradi ya uvuvi

Mwanza. Vijana 308 waliohitimu mafunzo ya programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT-Uvuvi) wamekabidhiwa Sh7 bilioni kwa ajili ya kuwawezesha kutekeleza miradi ya ufugaji wa samaki kwa vizimba, ufugaji wa jongoo bahari, kilimo cha mwani pamoja na unenepeshaji wa kaa, ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali kukabiliana na changamoto ya ajira. Akikabidhi hundi ya…

Read More

Naibu Waziri akabidhi viti mwendo 10 Manyara

Babati. Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Regina Ndege, amekabidhi viti mwendo kwa watu wenye mahitaji maalumu katika Wilaya ya Babati, ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kuwasaidia watu wenye ulemavu wa viungo kupata unafuu katika maisha yao ya kila siku. Akizungumza na Mwananchi Digital…

Read More

Sh1.7 bilioni zanufaisha vikundi 165 vya wanawake Mbarali

Mbarali. Katika kuhakikisha wanawake wanawezeshwa kiuchumi, Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya, imetoa zaidi ya Sh1.7 bilioni kwa vikundi 165 vya wanawake pekee. Hatua hiyo ni kutekeleza maelekezo ya Serikali, kuzitaka halmashauri nchini kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa makundi ya wajasiriamali wadogo, kwa lengo la kukuza uchumi wa kipato. Kauli hiyo imetolewa…

Read More

Takukuru yakabidhi mashine za Sh18 milioni kuokoa vichanga

Mwanza. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imekabidhi mashine mbili za matibabu, zenye thamani ya Sh18 milioni, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure, kwa ajili ya kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati na wale wanaopata ugonjwa wa manjano. Mashine hizo ni Radiant warmer, inayotumika kuwahudumia watoto wanaozaliwa…

Read More

Waongoza watalii watakiwa kuchukua tahadhari

Serengeti. Wakati Serikali ikiendelea kuchukua hatua za kukabiliana na athari za mvua zinazoendelea kunyesha, waongoza watalii wametakiwa kuchukua tahadhari wanazopewa na vikosi vya uokozi katika maeneo korofi katika Hifadhi ya Taifa Serengeti. Mamkala ya hifadhi hiyo imesema itaendelea kuhakikisha shughuli za utalii zinaendelea kama kawaida huku usalama wa watumiaji wa barabara, wakiwemo watalii, wanaowaongoza na…

Read More

Kyela yashusha mitambo kumaliza kero ya barabara

Mbeya. Kero ya miundombinu ya barabara iliyokuwa ikiwakabili wananchi wilayani Kyela mkoani Mbeya, huenda ikabaki historia baada ya Halmashauri hiyo kununua mitambo minne ya kisasa kwa ajili ya kukabiliana na changamoto hiyo kwa jamii. Mara kadhaa wananchi wilayani humo walikuwa wakiripoti kukumbwa na mafuriko kufuatia mitaro na mifereji kutiririsha maji na kusababisha kero kwenye makazi…

Read More

Polisi ilivyoweka kizuizi kongamano la siku ya wanawake Bawacha

Dar/mikoani. Vikwazo vimeendelea kuutawala mpango wa mkutano wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha) wa kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, baada ya makundi ya makada wao kuzuiwa na Jeshi la Polisi kwa nyakati tofauti wakiwa safarini kuelekea kwenye mkutano huo uliopangwa kufanyika Musoma, mkoani Mara, kesho Jumapili, Machi 8, 2026. Machi mosi, 2026, baraza hilo…

Read More