
Mvua yasababisha barabara Hifadhi ya Ngorongoro kufungwa kwa muda
Arusha. Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), imesema imefunga kwa muda baadhi ya barabara katika hifadhi hiyo kwa ajili ya matengenezo kutokana na kuharibiwa vibaya na nyingine kujaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Aprili 27, 2024 na Kaimu Meneja uhusiano wa umma wa mamlaka hiyo, Hamis Dambaya…