
Serikali ya Tanzania kufuta leseni za utafiti wa madini zisizofanyiwa kazi
Dodoma. Serikali ya Tanzania inakusudia kufanya mapitio ya leseni za utafiti wa madini ili kuzifuta zitakazobainika hazifanyi kazi au hazijalipiwa, lengo likiwa ni kutwaa maeneo na kugawa kwa wachimbaji wadogo. Hayo yamesemwa leo Alhamisi, Aprili 18, 2024 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akijibu swali la papo kwa hapo la Mbunge wa Kishapu (CCM), Boniphace…