
Sheria ya Magereza yatajwa chanzo cha manyanyaso kwa wafungwa
Dar/Morogoro. Kauli iliyotolewa na Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali, Mzee Nyamka kuhusu unyanyasaji wa wafungwa magerezani, imewaibua wadau wa haki za binadamu wakitaka Serikali iwajibike kuchukua hatua za haraka kwa kuwa mambo hayo yameshalalamikiwa sana. Wadau hao wakiwamo wanasheria, wameikosoa Sheria ya Magereza ya mwaka 1967 kuwa imepitwa na wakati na ndiyo chanzo…