Mbivu, mbichi suala la kikokotoo kujulikana Mei Mosi

Dodoma. Serikali imesema suala la kanuni mpya ya kikokotoo cha pensheni ya wastaafu lina maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan na limeanza kufanyiwa kazi, majibu yatajulikana kwenye sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi, jijini Arusha. Hayo yamesema leo Ijumaa Aprili 19, 2024 na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira…

Read More

Wafugaji Monduli walia bwawa kupasuka, kupoteza maji

Arusha. Wananchi wa jamii ya wafugaji katika kijiji cha Nanja kilichopo wilaya ya Monduli mkoani Arusha, wameiomba Serikali kuharakisha ukarabati wa kuta za bwawa la maji lililopo kijijini hapo, ambalo kuta zake zimevunjika na kusababisha maji mengi kupotea. Bwawa hilo la kuhifadhia maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kunyweshea mifugo, liliharibiwa na maji…

Read More

Mtoto adaiwa kujinyonga Arusha kisa kuchelewa shule

Arusha. Mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Olomitu iliyoko Chekereni jijini Arusha, Yusuph Zephania (13) anadaiwa kujinyonga hadi kufa kwa kuogopa adhabu itakayotolewa kwake baada ya kuchelewa shule. Tukio hilo limetokea jana April 18, 2024 nje ya nyumba katika kamba ya kuanikia nguo iliyokuwa nje. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, SACP…

Read More

Hizi hapa dalili za changamoto ya afya ya akili kwa mjamzito

Mwanza. Kukosa usingizi wakati wa ujauzito, kujilaumu, kuwaza sana, kula sana na wakati mwingine kutokula kabisa ni miongoni mwa mambo yanayotajwa kuwa dalili za changamoto ya afya ya akili kwa mjamzito. Dalili hizo zimebainishwa leo Ijumaa Aprili 19, 2024 wakati wa kufunga mafunzo kuhusu changamoto ya afya ya akili kwa wajawazito na kina mama waliojifungua…

Read More

Dk Nchimbi awaonya wanaCCM udalali kwa wasaka uongozi

Njombe. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi amewataka wanachama na viongozi wa chama hicho kujiepusha kuwa madalali wa watu wanaosaka nafasi za uongozi. Dk Nchimbi amesema kama kuna kitu kinachoweza kukidhoofisha chama hicho tawala ni viongozi kukubali kuwa madalali wa wagombea. “Mtu anayetaka kukufanya uwe dalali tafsiri yake ameshakupima, amegundua unanunulika,…

Read More

 Simbachawene amjibu Mpina | Mwananchi

Dodoma. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amemshukia mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina akimtaka kutodharauliana. Simbachawene amesema hayo leo Aprili 19, 2024 alipojibu hoja za wabunge walizotoa walipochangia bajeti ya ofisi yake kwa mwaka wa fedha 2024/25. Amesema nchi ambayo Mpina anasema imefeli inawezaje kutekeleza…

Read More

Watoto wa mitaani wafunguka wanayoyapitia

Arusha. Dharau, lugha za matusi na vipigo vya mara kwa mara wakati mwingine bila kosa, ni baadhi ya madhila wanayokumbana nayo watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani. Ili kuondokana na hilo, wameiomba Serikali kuwakusanya pamoja na kuwapatia elimu ya ujasiriamali, mikopo ya vijana hasa wale waliosogea umri. Wamesema lengo la kuhitaji kupatiwa mtaji ni waweze…

Read More