
Wenye nyumba Bonde la Msimbazi washtukiwa kutaka malipo ya wapangaji
Dar es Salaam. Wamiliki wa nyumba zinazoguswa na mradi wa uendelezaji Bonde la Mto Msimbazi wakiwa wameshalipwa fidia na kuanza kuhama, kumeibuka malalamiko ya waliokuwa wapangaji katika nyumba hizo kutolipwa licha ya Serikali kuwaahidi malipo. Kwa mujibu wa Serikali, malipo yamesitishwa kutokana na baadhi ya wahusika kubainika kughushi nyaraka. Katika utekelezaji wa mradi huo unaogharimu…