
Ajali za helikopta zinavyomaliza vigogo Kenya
Dar es Salaam. Ajali ya helikopta imeondoa uhai wa Mkuu wa Majeshi ya Kenya Jenerali Francis Ogolla leo Aprili 18, 2024. Mbali na Jenerali Ogolla, ajali hiyo pia imepoteza maofisa tisa, huku wengine wawili wakijeruhiwa. Wengine waliofariki katika ajali hiyo ni Brigedia Swaleh Said, Kanali Duncan Keitany, Luteni Kanali David Sawe, Meja George Benson Magondu…