Moravian yapata Askofu Mkuu, kuapishwa Juni 2

Mbeya. Aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo Kuu la Magharibi (KMT-JKM), Dk Alinikisa Cheyo amepata mrithi wake baada ya Mchungaji Robert Pangani kuteuliwa kushika nafasi hiyo. Mchungaji Pangani atasimikwa kukalia kiti hicho Juni 2 mwaka huu, huku Rais Samia Suluhu Hassan akitarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo. Mchungaji Pangani amechaguliwa na…

Read More

Mshitakiwa akana maelezo yake, adai hajui kilichomuua mkewe

Geita. Mshtakiwa Bahati Shija anayekabiliwa na shitaka la kumuua mkewe, Grace Daud kwa kumpiga na chuma kichwani ya  kukataa kurudiana naye, ameiambia Mahakama hajui sababu za kifo hicho. Kauli ya mshitakiwa huyo imekuja siku moja baada ya shahidi wa tatu, E.7719 Sajenti Pascal ambaye ni Askari Mpelelezi Wilaya ya Geita aliyerekodi maelezo ya onyo ya…

Read More

Serikali yaweka wazi juu uraia pacha

Ramadhan Hassan,Dodoma SERIKALI imesema haipo tayari kutumia uraia pacha ila hivi karibuni itaanza kutumia utaratibu wa hadhi maalum ambao utatoa fursa kwa wenye asili ya Tanzania waliopo nje kuchangia nchi yao. Hayo yameelezwa leo Alhamisi Aprili 18,2024 jijini hapa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika,Balozi Mbarouk Nasoro Mbarouk wakati akizungumza…

Read More

Namna makachero walivyomdaka mwizi wa bastola

Moshi. Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Benedicto Petro aliyeongoza timu ya makachero kuwakamata washtakiwa wa kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha, ameeleza namna walivyomkamata mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Eben Mwaipopo. Mshitakiwa huyo alikamatwa katika Kituo cha Basi cha Bomang’ombe wilayani Hai.  Shahidi ameeleza kuwa, katika mahojiano,  mshitakiwa aliwaeleza alipoificha silaha iliyotumika katika mauaji mkoani…

Read More

Waziri asimulia alivyosaidiwa kusomeshwa na Sokoine

Arusha. “Siku zote nimekuwa nikiamini huyu baba mzalendo wa kweli amekuwa na dhamana kubwa katika maisha yangu, naona Mungu alimtuma ninyanyuke katika familia yetu ya watoto saba,  hakuna mwingine aliyeenda shule zaidi yangu.” Ni nadra kwa kiongozi ambaye amepata mafanikio ya kielimu, kiuchumi na kisiasa kuelezea mapito aliyopitia, lakini si kwa Naibu Waziri wa Madini,…

Read More

Mbowe, Lissu watakavyoongoza maandamano ya amani Chadema

Dar es Salaam. Ikiwa zimepita siku 54 baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kufanya maandamano ya amani katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha, imeandaa mengine ya nchi nzima. Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Makamu Mwenyekiti -Bara, Tundu Lissu watashiriki maandamano hayo na ratiba imetolewa ikieleza namna watakavyoyaongoza….

Read More