Kizungumkuti ununuzi magari ya ma-RC, DC

Dar es Salaam. Wakati Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Seriali za Mitaa (Tamisemi),  ikipanga kutumia Sh190.57 bilioni kwa ajili ya ununuzi wa magari ya viongozi wa mikoa na wilaya, suala hilo limeibua hisia tofauti miongoni mwa wananchi, wengine wakiona ni mwendelezo wa matumizi mabaya ya fedha za umma. Kwa upande mwingine, baadhi ya…

Read More

BoT kutoa elimu ya fedha shuleni

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital Benki Kuu ya Tanzania(BoT) imedhamiria kutoa elimu ya fedha kuanzia ngazi ya elimu msingi hadi vyuo vikuu kuwawezesha vijana kuwa na uwezo wa nidhamu ya kusimamia fedha. Hayo amesemwa leo Aprili 17, 2024 jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga wakati…

Read More

Mwongozo kwa wanaojitolea waja | Mwananchi

Dodoma. Serikali ya Tanzania inakamilisha mwongozo kwa vijana wanaojitolea utakaiwawezesha kupatiwa malipo wakati wa utumishi wao. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amesema hayo leo Alhamisi Aprili 18, 2024 wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Momba (CCM), Condester Sichalwe. Katika swali la nyongeza, Sichalwe…

Read More

BAJETI YA TAMISEMI YAWAPA MATUMAINI WANAHARAKATI WA JINSIA – MWANAHARAKATI MZALENDO

ONGEZEKO la fedha shilingi Trilioni 10 kwenye bajeti ya Wizara ya Tamisemi imeibua matumaini kwa Wanaharakati wa masuala ya kijinsia ambapo wanatarajia itakwenda kutoa chachu ya kuinua ushiriki wa wanawake katika masuala ya uongozi na kuwaepusha na vitendo vya ukatili, unyanyasaji na kuwaondolea mazingira magumu wakati wa uchaguzi. Hayo yamesemwa leo April 17,2024 katika Semina…

Read More

Muhimbili yapokea mashine ya uchunguzi saratani ya matiti

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH) imepokea mashine maalumu Mammography aina ya Senographe Pristina 3D yenye thamani ya milioni 800 kwa ajili ya kufanya uchuguzi wa saratani ya matiti. Pia machine hiyo itatumika katika kuwafundishia wataalam na kufanya tafiti mbalimbali. Akizungumza katika hafla ya kupokea mashine hiyo leo Aprili 17, 2024 Dk.Hamad…

Read More

Mwanafunzi wa Chuo cha Mtakatifu Joseph kuzikwa leo

Morogoro.  Mwanafunzi  Hajirath Shaban aliyeuawa kwa kuchomwa kisu na watu wasiojulikana usiku wa Aprili 16 alipokuwa hosteli, anatarajia kuzikwa leo Aprili 18, 2024 kwenye makaburi ya Kola Manispaa ya Morogoro. Mwanafunzi huyo aliyekuwa akisoma Chuo cha Mtakatifu Joseph kilichopo Manispaa ya Morogoro, aliuawa baada ya kuvamiwa akiwa hosteli za chuo hicho zilizopo Mkundi, Aprili 16,…

Read More

Walimu wa kujitolea waula Dar

Na Nora Damian, Mtanzania Digital Walimu 150 wa masomo ya sayansi waliokuwa wakijitolea katika shule mbalimbali za sekondari za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wamepewa ajira za mkataba kukabili upungufu uliopo. Juni 2023 Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ilitoa mwongozo unaoelekeza kuwatumia walimu waliohitimu vyuo ambao bado hawajaajiriwa ili kuboresha…

Read More

Takukuru Geita yabaini kasoro kwenye miradi 1,800

Geita. Miradi 1,800 yenye thamani ya Sh7 bilioni iliyofuatiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Geita mwaka 2022/23 imebainika kuwa na kasoro zikiwamo za usanifu, ununuzi na baadhi ya fedha za miradi kuhamishiwa kwenye matumizi yasiyohusiana na mradi husika. Hayo yamebainishwa leo Aprili 18, 2024 kwenye kongamano maalumu linaloendelea mjini Geita…

Read More