
Petroli yaanza kupatikana, hofu bado Unguja
Unguja. Licha ya huduma ya mafuta ya petrol kuanza kupatikana usiku wa kuamkia leo Jumatano, Aprili 17, 2024 kisiwani Unguja, bado hofu imeendelea kuibuka kutokana na kiasi kidogo kinachodaiwa kupatikana. Kwa takribani siku tatu kuanzia Aprili 14 hadi Aprili 16 Unguja ilikabiliwa na upungufu wa petroli katika vituo vingi vya mafuta, kusababisha adha kwa wananchi…