Majaliwa aagiza mrejesho wa michango ya maafa kwa jamii
Dodoma. Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kutekeleza wajibu wao wa kutoa mrejesho kwa jamii juu ya michango, kazi zilizofanyika na kiasi cha fedha kilichotumika katika maafa pindi yanapojitokeza. Majaliwa amesema hayo leo Alhamisi Aprili 18, 2024 wakati akijibu swali la papo kwa hapo kwa Mbunge wa viti maalumu…