Video: Polisi Yapiga Marufuku Maandamano ya Desemba 9, Yasifanyike Nchi Nzima
Jeshi la Polisi Tanzania limepiga marufuku “maandamano ya amani yasiyo na kikomo,” yaliyotangazwa kufanyika Desemba 9, 2025, likisema yamekosa sifa za kisheria na yanaashiria mipango ya uhalifu unaoweza kuhatarisha usalama wa taifa. Katika taarifa iliyotolewa Desemba 5, 2025 na Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David Misime, jeshi hilo limesema…