‘Acheni dhana potofu kuhusu tohara’

Musoma. Wakazi wa Mkoa wa Mara wametakiwa kuachana na dhana kuwa mtoto wa kiume akifanyiwa tohara katika umri mdogo uume wake utakuwa mdogo, badala yake wafanye tohara mapema ili kujiepusha na magonjwa vikiwamo Virusi vya Ukimwi (VVU). Wito huo umetolewa mjini hapa leo Ijumaa Mei 10, 2024 na Mratibu wa Upimaji wa VVU na Huduma…

Read More

UTARATIBU WA BIMA YA AFYA NI KUCHANGIANA SIO MSAADA

Serikali kupitia Wizara ya Afya imesema kuanza kutekelezwa kwa Bima ya Afya kwa wote itakuwa suluhisho la kudumu la kurahisisha upatikanaji wa huduma za Afya kwa makundi yote nchini ikiwemo wanafunzi Kauli hiyo imebainishwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel leo Jijini Dodoma wakati akijibu swali Namba 305 kutoka kwa Mbunge wa Sikonge,…

Read More

Wachimbaji waendelea kuiangukia Serikali mbadala wa zebaki

Butiama. Wachimbaji wadogo wa dhahabu katika mgodi wa dhahabu wa Buhemba wilayani hapa,  wameiomba Serikali kuwaletea njia mbadala ili kuondokana na matumizi ya zebaki katika uchimbaji wao. Wachimbaji hao wamesema kwa muda mrefu Serikali imekuwa ikieleza juu ya uwepo wa madhara ya kiafya ya moja kwa moja kwa watumiaji wa zebaki pamoja na mazingira, lakini…

Read More

Zoezi la sensa Uganda laanza na malalamiko ya wafanyakazi – DW – 10.05.2024

Baadhi ya maafisa walioshiriki mafunzo ya  kuendesha zoezi la sensa Uganda ambalo limeanza Alhamisi usiku wanalalamika kuwa hawajapokea vitendea kazi ikiwemo kifaa cha kidijitali cha kurikodi taarifa kutoka kwa raia. Isitoshe hawana sare wala vitambulisho kuweza kukaribishwa majumbani mwa watu ambao wamesalia makwao wakisubiri kuhesabiwa.  Serikali ilitangaza Ijumaa kuwa siku ya mapumziko kwa ajili ya sensa. Soma…

Read More

DC James ashangaa udumavu wilaya yenye vyakula tele

Iringa. Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Kheri James amesema tatizo la udumavu kwenye wilaya hiyo halitokani na uhaba wa vyakula isipokuwa mpangilio mbovu wa ulaji. Amesema ni aibu kuitwa mkuu wa wilaya kwenye eneo lenye vyakula vya kutosha lakini udumavu ni mkubwa. James amesema hayo jana Mei 9, 2024 kwenye maadhimisho ya Siku ya Mkulima…

Read More