Mapya yaibuka mwanafunzi aliyepotea, mwili kukutwa kwenye shimo la choo
Kibaha. Wakati familia ya mwanafunzi Angel John aliyekutwa amekufa ndani ya shimo la choo Kibaha, mkoani Pwani, ikiendelea na taratibu za mazishi, Polisi limesema kuna uwezekano mkubwa kuwa aliuawa. Kutokana na hilo, Polisi limesema linawasaka waliohusika wa mauaji ya mtoto huyo mwenye miaka minane. Angel aliyekuwa akisoma darasa la pili katika Shule ya Msingi Carisa…