UBALOZI WA MAREKANI KUENDELEZA MASHIRIKIANO NA CHUO CHA MIPANGO DODOMA
Na Mwandishi Wetu, Dodoma. BALOZI wa Marekani nchini Tanzania, Michael Anthony Battle amesema Serikali yake itaendelea kuimarisha uhusiano wa kikazi na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) ili kuchochea kasi na juhudi ya Serikali ya Tanzania katika kutokomeza umaskini. Ameeleza kufurahishwa na namna ya kitaalamu na kizalendo ambayo chuo hicho kimekuwa kikitekeleza programu mbalimbali…