Shamrashamra za Kilele cha Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Aprili, 2024

Maonesho ya Kwata ya Kikundi cha Askari wa Jeshi la Polisi Tanzania kutoka Zanzibar Maarufu kama Askari wa Tarabushi wakionesha Maonesho mbalimbali ya aina ya Kwata tangu kipindi cha utawala wa Sultan na kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Askari hao walijipatia umaarufu mkubwa kutokana na uvaaji wa Kofia zao za Tarabushi.  Onesho hilo…

Read More

Ukuta wa nyumba waua watoto watatu wa familia moja

Shinyanga. Mvua zinazoendelea kunyesha katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga mkoani hapa, zimesababisha vifo vya watoto watatu wa familia moja katika Kitongoji cha Miembeni B, Kijiji cha Mishepo baada ya kuangukiwa na nyumba waliyokuwa wamelala usiku wa kuamkia leo. Akisimulia tukio hilo leo Ijumaa Aprili 26, 2024, mama wa watoto hao, Joyce Nchimbi ambaye amenusurika…

Read More

MSAJILI WA HAZINA AZUNGUMZA NA MKURUGENZI MPYA WA HESLB

Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu (kulia), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Dkt. Bill Kiwia (wa pili kushoto), katika kikao kilichofanyika Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Dkt. Bill Kiwia (kushoto), akizungumza alipokuwa akitoa wasilisho lake kwa…

Read More

‘Uelewa mdogo chanzo cha wakulima kutotumia mbolea’

Mwanza. Kampuni za kuuza mbolea nchini zimetakiwa kutoa elimu kwa wakulima kupitia mashamba darasa ili kuwashawishi matumizi ya mbolea shambani yanayotajwa kua chini mikoa ya kanda ya ziwa. Akizungumza leo Ijumaa Aprili 26, 2024 wakati wa mkutano wa kuwajengea uwezo mawakala wa mbolea ya Minjingu Kanda ya Ziwa, Meneja wa Kanda wa Mamlaka ya Udhibiti…

Read More

Mkakati wa Serikali kunusuru wanafunzi na mafuriko

Dar es Salaam. Mvua inayoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini na kusababisha uharibifu wa mali, makazi na miundombinu ya barabara na majengo, imeifanya Serikali kuchukua uamuzi mgumu wa kuzitaka shule zote zilizoathiriwa na mvua hizo kufungwa. Uamuzi huo unachukuliwa kipindi ambacho imeshuhudiwa mvua hizo za El-Nino tangu zilipoanza Oktoba mwaka jana kusababisha vifo vya watu zaidi…

Read More

Mikoa 16 kupata mvua leo, upepo mkali wa siku nne

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema baadhi ya maeneo katika mikoa 16 ya Tanzania bara na visiwa na Unguja na Pemba zitashuhudia mvua kubwa leo Ijumaa, Aprili 26, 2024. Mikoa hiyo ni Dar es Salaam, Tanga, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Shinyanga, Simivu,…

Read More