Masache aomba kuunganishwa barabara Makongorosi-Tabora akiomba kura za Urais

Mbeya. Mgombea pekee ubunge Jimbo la Lupa, Wilaya ya Chunya Masache Kasaka ameomba mgombea Urais atakapoapishwa na kuunda Serikali, kuboresha miundombinu barabara kutoka Makongorosi ili kuunganisha shughuli za kiuchumi baina ya Mkoa wa Mbeya ya Tabora. Mbali na Ombi hilo pia Masache ameomba maeneo ya wachimbaji wadogo kufikishiwa nishati ya umeme kufuatia wananchi wake kujikita…

Read More

Wanafunzi Watanzania washinda tuzo ya teknolojia duniani

Dar es Salaam. Timu ya wanafunzi sita kutoka vyuo vikuu vitatu vya Tanzania imeshinda mashindano ya kimataifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT), ikiibuka kidedea dhidi ya timu 167 kutoka nchi 48 duniani. Wanafunzi hao waliowakilisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), na Taasisi ya Teknolojia Dar es…

Read More

Daraja dogo la mbao chakavu lawatesa wanakijiji Hai

Hai. Wananchi wa Kijiji cha Kyuu, Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, wameiomba Serikali kuchukua hatua za haraka kujenga daraja dogo katika eneo la Mto Kishenge, Kitongoji cha Maiputa, ili kuwawezesha kuendelea na shughuli mbalimbali za kijamii na kimaendeleo bila vikwazo. Ombi hilo limetolewa wakati wa ziara ya Ofisa Tarafa wa Masama, Nswajigwa Ndagile, alipotembelea eneo…

Read More

Jela miaka 15 kwa kumuua mkewe kwa mchi bila kukusudia

Arusha. Mahakama Kuu Masijala Ndogo ya Mtwara, imemhukumu adhabu ya kifungo cha miaka 15 jela, Shaibu Mtavira, baada ya kumkuta na hatia ya kumuua bila kukusudia mkewe, Aziza Mtelia, kwa kumpiga na mchi kisha kumzika kwenye shamba lao. Shaibu alikiri kumuua mkewe baada ya kutokea kutokuelewana  katika mazungumzo yao na kusababisha mapigano kati yao ambapo…

Read More

Chaumma yaomba kura wanachama wa Chadema, yaeleza kuwaletea ‘reforms’

Morogoro. Mgombea mwenza wa urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Devotha Minja amewaomba wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kukichagua chama hicho ili mabadiliko ya sheria za uchaguzi ‘reforms’ ambazo wanazipigania wakaziharakishe. Devotha amesema hata wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanapaswa kuichagua Chaumma ili ikabadili mifumo ya kodi ambayo sio…

Read More