JKCI yaokoa Sh1.2 bilioni kwa kutibu watoto 40 nchini

Dar es Salaam. Upasuaji wa watoto 40 wenye matatizo ya kuzaliwa nayo ya moyo uliofanyika kwa siku nane nchini umeokoa Sh1.2 bilioni ambazo zingetumika kama wangetibiwa nje ya nchi. Madaktari wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka nchini Uingereza kesho Aprili 26, wanahitimisha siku nane za upasuaji wa watoto…

Read More

MWENGE WA UHURU KUINGIA MKOA WA PWANI APRILI 29

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge akizungumza  na Waandishi wa Habari  Ofisini kwake leo Aprili  25, 2024 hawapo pichani. Na Khadija Kalili, Michuzi Tv MKUU wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge ametoa ratiba ya kuukimbiza Mwenye wa Uhuru ambao utaingia Mkoa wa Pwani Aprili 29 ukitokea Mkoa wa Morogoro. Akizungumza katika mkutano…

Read More

Watu wanne wafariki dunia ajali ya moto Kagera

Kagera. Watu wanne wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa katika ajali ya moto baada ya nyumba waliyokuwa wanaishi kuungua moto unaodaiwa kusababishwa na mafuta ya petroli yaliyokuwa yamehifadhiwa kwenye madumu. Ajali hiyo imetokea alfajiri leo Aprili 25, 2024 katika Kata ya Rusumo, Wilaya ya Ngara mkoani Kagera kwenye nyumba ya Dominick Didas, yenye vyumba vinne…

Read More

Tanzania na Urusi Kushirikiana Kudhibiti Uhalifu wa Kimtandao

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu wa wizara hiyo, Miriam Mmbaga(wapili kushoto) wakisikiliza ufafanuzi wa programu maalumu ya kudhibiti uhalifu wa Kimtandao kutoka kwa Meneja Mauzo wa Kampuni ya SOLAR,Timul Solovev wakati wa Maonesho ya Teknolojia ya Kudhibiti Uhalifu huo yanayoendelea katika Ukumbi…

Read More

S.H. Amon apoteza umiliki jumba la ghorofa nane Kariakoo

Dar es Salaam. Mahakama ya Rufani imekazia uamuzi wake wa awali unaomuondolea mfanyabiashara Sauli Amon, maarufu S.H. Amon umiliki wa jumba la ghorofa nane alilojenga eneo la Kariakoo, Dar es Salaam. Jumba hilo lipo katika kiwanja alichonunua nyumba awali. Uamuzi huo unatokana na shauri la maombi ya marejeo alilolifungua S.H. Amon, akipinga hukumu ya Mahakama…

Read More

TFS WACHANGIA MIL.20 KWA WENYE MAAFA KIBITI NARUFIJI

Na Khadija Kalili ,Michuzi Tv MKUU wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge leo amepokea hundi yenye thamani ya Mil.20 kutoka Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) ikiwa ni katika muendelezo wa kuchangia watu wa Kibiti na Rufiji ambao wamepata changamoto ya mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea nchini kote. Imeelezwa na Afisa Uhusiano wa TFS Johary…

Read More

UCSAF yapongezwa kwa kujenga na kuhamia Dodoma

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ameupongeza Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote(UCSAF) kwa kutekeleza maelekezo ya Serikali kwa taasisi za umma kujenga na kuhamia katika Makao Makuu ya nchi Dodoma. Akizungumza kabla ya kuzindua rasmi jengo la Ofisi za Makao Makuu ya UCSAF leo Aprili 25, 2024…

Read More

Vifo vilivyosababishwa na mafuriko Moshi vyafikia saba

Moshi. Vifo vinavyotokana na mafuriko katika Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro vimeongezeka na kufikia saba, baada ya mtu mmoja kufariki kwa kuangukiwa na kifusi katika eneo la Mbokomu na mwingine aliyekuwa majeruhi kufariki dunia. Katika ya vifo hivyo, wamo pia watu wanne wa familia moja wakiwemo watoto watatu ambao wamepoteza maisha baada ya kuangukiwa na…

Read More