Rais kuteua ma-DED ngoma nzito
Dar es Salaam. Kauli ya Mbunge wa Mlimba (CCM), Godwin Kunambi ya kuhoji sababu za wakurugenzi wa halmashauri kuendelea kuteuliwa na Rais, imewaibua wadau wakisema nafasi hizo ziombwe kulingana na sifa zitakazowekwa. Suala la uteuzi wa wakurugenzi wa halmashauri, limekuwa likilalamikiwa na wadau na hasa baadhi ya vyama vya upinzani, vikidai kuwa nafasi hizo zinatumika…