Wanazuoni, wataalamu waeleza faida, changamoto na maadui wa Muungano
Unguja. Wakati Tanzania ikielekea kuadhimishwa miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, zimetajwa changamoto, faida na maadui wa Muungano huo ulioasisiwa mwaka 1964. Miongoni mwa faida za Muungano ni kupanua maeneo ya kiuchumi, heshima kimataifa, amani, umoja na masuala ya ulinzi na usalama katika mataifa hayo mawili. Changamoto kubwa ni kutoundwa tume ya akaunti…