Mbunge ataka wanaofanya biashara na watoto watafutiwe maeneo
Dodoma. Mbunge wa Viti Maalumu Janeth Mahawanga amehoji iwapo Serikali haioni umuhimu wa kuwatafutia maeneo wanawake wenye watoto wadogo wajasiriamali wanaofanya biashara zao pembezoni mwa barabara wakati wakisubiri kuwatengea maeneo husika. Akiuliza maswali ya nyongeza bungeni leo Ijumaa Aprili 19, 2024, Janeth pia amehoji lini Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kitatengeneza programu mahususi kwa ajili…