CDF wa Kenya afariki dunia katika ajali ya helkopta

Dar es Salaam. Rais wa Kenya, William Ruto amethibitisha kifo cha Mkuu wa Majeshi ya nchi hiyo (CDF), Jenerali Francis Ogolla aliyefariki dunia katika ajali ya helikopta iliyotokea leo Aprili 18, 2024 eneo la Algeyo katika Kaunti ya Marakwet. Mbali na Jenerali Ogolla, ajali hiyo iliyotokea leo saa 8.20 mchana pia imesababisha vifo vya maofisa…

Read More

Biashara Tanzania na Uturuki kufikia Sh2.58 trilioni

Dar es Salaam. Tanzania na Uturuki zimekubaliana kukuza biashara ya pamoja hadi kufikia Sh2.58 trilioni kutoka Sh890 bilioni iliyopo sasa. Wakati azma hiyo ikiwemo hiyo ikiwekwa, mikataba sita ya makubaliano kati ya nchi hizo mbili imesainiwa ambapo miongoni mwake inalenga kukuza diplomasia ya kiuchumi na elimu ya juu. Hayo yamebainishwa katika mkutano wa pamoja kati…

Read More

Ajali za helikopta zinavyomaliza vigogo Kenya

Dar es Salaam. Ajali ya helikopta imeondoa uhai wa Mkuu wa Majeshi ya Kenya Jenerali Francis Ogolla leo Aprili 18, 2024. Mbali na Jenerali Ogolla, ajali hiyo pia imepoteza maofisa tisa, huku wengine wawili wakijeruhiwa. Wengine waliofariki katika ajali hiyo ni Brigedia Swaleh Said, Kanali Duncan Keitany, Luteni Kanali David Sawe, Meja George Benson Magondu…

Read More

Asasi ya Agenda yabainisha madhara ya kemikali zilizopo kwenye Plastiki

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizojiunga katika kupunguza matumizi ya plastiki kama njia mojawapo ya kutunza na kuhifadhi mazingira. Katika kutekeleza suala hilo Juni mosi mwaka 2019 Tanzania ilitangaza marufuku ya kutengeneza, kusambaza, kutumia au kutunza mifuko ya plastiki. Katazo hili lilifuatia tangazo lililotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waziri wa…

Read More

Wananchi wafunguka mauaji ya mwanafunzi wakati akizikwa

Morogoro.  Maziko ya mwanafunzi wa Chuo cha Mtakatifu Joseph aliyeuawa juzi kwa kuchomwa kisu na mtu asiyejulikana akiwa kwenye eneo la hosteli za chuo hicho, yamefanyika katika makaburi ya Kola, Morogoro. Wakizungumza Leo Alhamisi Aprili 18, 2024 baada ya maziko hayo, baadhi ya waombolezaji wameliomba Jeshi la Polisi mkoani Morogoro  kuhakikisha linamtia mbaroni muuaji. Hajrat…

Read More

Wananchi wafunguka mauaji ya mwanafunzi wakati akizwa

Morogoro.  Maziko ya mwanafunzi wa Chuo cha Mtakatifu Joseph aliyeuawa juzi kwa kuchomwa kisu na mtu asiyejulikana akiwa kwenye eneo la hosteli za chuo hicho, yamefanyika katika makaburi ya Kola, Morogoro. Wakizungumza Leo Alhamisi Aprili 18, 2024 baada ya maziko hayo, baadhi ya waombolezaji wameliomba Jeshi la Polisi mkoani Morogoro  kuhakikisha linamtia mbaroni muuaji. Hajrat…

Read More

Dk Biteko atoa kauli usalama Bwawa la Julius Nyerere

Dodoma. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amesema licha mvua zinazoendelea kunyesha nchini, Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) lipo salama kwasababu limejengwa kisayansi. Mbali na hilo, amesema bwawa hilo linaendelea kuzalisha umeme kupitia mtambo namba tisa huku mitambo mingine miwili ikiwa ukingoni kukamilika. Amesema hayo leo Alhamisi Aprili…

Read More

Muuza maji aliwa na mamba ziwani

Mwanza. Muuza maji na mkazi wa Kijiji cha Busisi Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza aliyefahamika kwa jina moja la Charles, anadaiwa katoweka ziwani baada ya kupitiwa na mamba alipokuwa akichota maji Ziwa Victoria. Tukio hilo limetokea jana Aprili 17, 2024 saa 1:30 usiku akiwa anachoya maji ziwani katika eneo hilo lililopo karibu na mradi wa…

Read More

Wizara yataka wanawake kugombea kwa wingi uchaguzi ujao

Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Mwanaidi Ali Khamis amewataka wanawake kujitokeza kwa wingi kuwania uongozi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani ili kufanikisha malengo ya kuwa na usawa wa kijinsia katika nafasi za uongozi. Tanzania ambayo kwa sasa inaongozwa na Rais mwanamke…

Read More