Kaya saba zakosa makazi, Mto Kiwira ukiporomosha udongo
Mbeya. Maisha ya wananchi wilayani Rungwe Mkoa wa Mbeya yako hatarini, baada ya maji ya Mto Kiwira kumong’onyoa udongo na kuharibu barabara inayounganisha vijiji Kapugi na Lyenje na nyumba saba, huku nyingine 34 zikiwa hatarini. Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Huniu amewataka wananchi wa kijiji cha Lwenje kuchukua tahadhari na…