
ZAIDI YA WATEJA 1,000 WAREJESHEWA HUDUMA YA MAJI NDANI YA OFA MAALUMU YA SOUWASA
Songea_Ruvuma. Meneja Huduma kwa Wateja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA), Jumanne Gayo, amesema zaidi ya wateja 1,000 kati ya 2,000 waliokuwa wamesitishiwa huduma ya maji kutokana na madeni, tayari wameunganishwa tena na huduma hiyo kupitia ofa maalum ya urejeshaji huduma iliyoanza Agosti 4, 2025. Akizungumza leo Septemba 4, 2025, …