Kamanda Mallya aagwa, Chongolo amtabiria makubwa

Songwe. “Heshimu kazi, penda watu na siyo vitu”. Hayo ni maneno ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Theopista Mallya kwa askari wa Songwe wakati akiagwa rasmi katika mkoa wa Songwe ambako alihudumu pia katika nafasi hiyo kabla ya kuhamishiwa Dodoma. Machi 14, 2024, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camilius Wambura aliwabadilisha vituo…

Read More

Serikali yatoa sababu kukatika kwa umeme

Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Nishati nchini Tanzania, Judith Kapinga amesema changamoto ya kukatika kwa umeme inayojitokeza katika baadhi ya maeneo, inasababishwa na uchakavu wa miundombinu. Uchakavu huo kwa mujibu wa Kapinga umetokana na miundombinu hiyo kutumika kwa muda mrefu, huku akifafanua Serikali ipo katika hatua ya kuiboresha. Kapinga ametoa kauli hiyo juzi Jumamosi…

Read More

SMZ kupima kupima utendaji kazi watumishi kidijitali

Unguja. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), itaanza kutumia Mfumo wa Kielektroniki wa Upimaji Utendaji Kazi (PA) ili kuongeza ufanisi katika taasisi za umma. Kwa sasa Serikali inatumia fomu ya upimaji utendaji kazi (PAF) kuwapima watumishi wa taasisi za umma, ambapo utekelezaji wake ulianza tangu Novemba 2019 hadi sasa unaendelea. Hayo yameelezwa na Waziri wa…

Read More

TUNA MKAKATI MAALUM NA COMORO- Prof JANABI

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,Prof Mohamed Janabi amesema kuwa wana mkakati maalum wa kutoa huduma za kisada za tiba kwa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kutoka visiwa vya Comoro kutokana na ongezeko la idadi yao katika siku za karibuni. Prof Janabi alisema hayo alipokuwa akizungumza na Balozi Mteule wa Tanzania nchini Comoro,Saidi Yakubu…

Read More

Kiongozi Mkuu Iran amteua mrithi wa Rais Ebrahim

Kiongozi wa ngazi ya juu nchini Iran, Ayatollah Ali Khamenei, amemteua makamu wa kwanza wa rais wa Iran, Mohammad Mokhber, kuwa rais kufuatia kifo cha Rais Ebrahim Raisi katika ajali ya helikopta. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea). Makamu huyo wa rais amechukua madaraka hayo ikiwa zimesalia siku 50 kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu nchini…

Read More

Watumishi 85,471 walioenguliwa kipindi cha JPM wapandishwa vyeo

SERIKALI imesema kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 hadi sasa jumla ya watumishi 375,904 wamepandishwa vyeo wakiwemo watumishi 85,471 walioathirika na zoezi la uhakiki katika kipindi cha uongozi wa Serikali ya Hayati John Magufuli. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). Aidha, imewaagiza waajiri wote kupeleka taarifa za madeni ya watumishi ambao waliathiriwa na uhakiki uliofanyika katika kipindi…

Read More

Huyu ndiye Rais wa mpito wa Iran

Wakati taratibu za mazishi ya Rais wa Iran, Ebrahim Raisi zikiendelea, Makamu wa Rais Mohammad Mokhber anayetarajiwa kurithi nafasi hiyo kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo, ameongoza mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri.Raisi amefariki kwenye ajali ya helikopta jana Mei 19, 2024 akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo…

Read More