Wanaume 17, 694 washiriki kupeleka wake zao kliniki
Unguja. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema kuwa kinababa 17,694 sawa na asilimia 34 ya kinamama wote waliokwenda kliniki ya afya ya uzazi na mtoto walishiriki kuwapeleka wenza wao kupata huduma za afya ya uzazi na mtoto wakati wa ujauzito. Hayo yamebainika leo Mei 17, 2024 katika mkutano wa 15 wa Baraza la Wawakilishi Chukwani…