Bajeti ya uchaguzi, kulinda haki za raia

Dodoma. Nyongeza ya fedha kwenye bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani, imelenga kuwezesha utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai. Pia bajeti hiyo imelenga kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuliwezesha Jeshi la Polisi kutimiza majukumu yake, ikiwemo la uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani. Maombi ya…

Read More

Apandishwa kizimbani akidaiwa kumbaka mtoto wa miaka 17

Geita. Mkazi wa Mgusu Mjini Geita Magongo Kulwa (30) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Geita akidaiwa kumbaka mtoto wa miaka 17.  Mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo, Nyakato Bigirwa, Mwendesha mashtaka Luciana Shaban amesema mshtakiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 4, 2024 huko Mgusu. Hata hivyo, mshtakiwa huyo alikana kutenda kosa hilo na…

Read More

Mbunge aliyetaka pasipoti kuingia Zanzibaar azua jipya

Dodoma. Mbunge wa Konde (ACT-Wazalendo), Mohamed Said Issa aliyetaka wananchi wa Tanzania Bara (Watanganyika) waingie Zanzibar kwa pasipoti, amezua lingine la ubaguzi akikataa taarifa tatu za kumtambua yeye ni Mtanzania. Hayo yametokea bungeni leo Mei 15, 2024 wakati wa mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani kwa mwaka wa…

Read More

TRA yaja na kibano kwa wanaokwepa kutoa risiti

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetengeneza mfumo unaozifuatilia mashine za kutoa risiti za kielektroniki (EFD) ikisema ndio mwarobaini wa wafanyabiashara wanaokwepa kutumia mashine hizo.  Kupitia mfumo huo, utendaji wa mashine zote za EFD zitafuatiliwa na pale itakapoonekana kuna kusuasua kwenye utoaji wa risiti, mfanyabiashara anayemiliki mashine husika atatafutwa na hatua za kisheria…

Read More

Polisi, TCRA waendelea kuwasaka ‘tuma kwa namba hii’

Dar es Salaam. Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) limewakamata na kuwahoji watu 27 kwa tuhuma za makosa ya kimtandao yakiwamo ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu. Idadi hiyo inafikisha jumla ya watuhumiwa 83 waliokamatwa tangu kuanza kwa operesheni ya kuwasaka miezi mitatu iliyopita. Baadhi…

Read More

Wanaodaiwa kumlawiti mtoto wa miaka mitatu mbaroni Arusha

Arusha. Watu ambao idadi yao haikutajwa wanaotuhumiwa kumlawiti mtoto wa miaka mitatu katika Kata ya Muriet, jijini Arusha wamekamatwa.  Kukamatwa kwao kunatokana na agizo la Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda alilolitoa mwishoni mwa wiki wakati akihitimisha siku tatu za kliniki ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi. Makonda alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya…

Read More