Mashimo ya viraka barabarani yawatesa madeva
Dar/Mikoani. Hivi unajua shimo la barabara linapochongwa ili kuwekwa kiraka linapaswa lidumu kwa saa 72 tu kabla ya kuzibwa? Si hivyo tu, hata barabara inapokatwa kwa ajili ya kuwekwa kiraka, utekelezwaji wake unapaswa kufanyika kwa muda usiozidi saa 48. Kwa mujibu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), uwekaji wa kiraka ni mbinu ya dharura inayofanywa…