Israel yatwaa udhibiti wa mpaka wa Rafah – DW – 07.05.2024
Mapema asubuhi ya Jumanne (Mei 7), jeshi la Israel lilipeleka vifaru kadhaa kwenye mji wa kusini mwa Gaza, Rafah, ikiwa ni siku moja tu baada ya kuwaonya Wapalestina wanaoishi huko kuhama kabla ya operesheni ya ardhini kuanza. Picha za vidio zilizosambazwa na jeshi hilo zilionesha vifaru vikipeperusha bendera ya Israel na vikitwaa udhibiti wa mpaka…