Wahamiaji haramu 10,960 wakamatwa wakiingia nchini, RC Mwassa akerwa

Bukoba. Idara ya uhamiaji mkoani Kagera imefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 10,960 wakiingia nchini kinyemela kuanzia Januari hadi Septemba 2025. Akizungumza na Mwananchi Digital, Septemba 3, 2025 ofisa Uhamiaji Mkoa wa Kagera, Mrakibu mwandamizi, Eleneus Kasimbazi amesema idara hiyo ya uhamiaji Mkoa wa Kagera kupitia doria mbalimbali walizozifanya kwenye maeneo muhimu ya mipaka ya nchi jirani…

Read More

Udsm, China waanzisha kituo cha elimu ya kidijitali kwa walimu

Dar es Salaam. Katika kuelekea maendeleo ya elimu kwa kutumia teknolojia ya kidijitali, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm) kwa kushirikina na Chuo Kikuu cha  Zhejiang Normal cha nchini China, wamefungua Kituo cha ushirikiano wa elimu ya kidijitali mahususi kwa ajili ya kuwapatia mafunzo walimu. Kituo hicho kitakachoitwa ‘China-Africa Regional Centre for Digital Education…

Read More

Waliokuwa watumishi Kigamboni wapandishwa kizimbani

Dar es Salaam. Aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Fedha na Mhasibu wa Manispaa ya Kigamboni, Jonathan Manguli (38) na wenzake 12, wakiwamo wafanyabiashara wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashtaka 10, yakiwamo ya kuchepusha fedha na kuisababishia Wizara ya Tamisemi hasara ya Sh165 milioni. Washtakiwa wengine waliokuwa watumishi wa manispaa hiyo ni mhasibu Godfrey Martiny (44), mkuu…

Read More

Mgombea urais Chaumma aahidi pensheni kwa wazee wote akiwa rais

Tanga. Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Salum Mwalimu ameahidi kuanzisha mpango wa pensheni ya kila mwezi kwa wazee wote nchini, iwapo atachaguliwa kuwa rais katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025. Mwalimu amesema wazee ni rasilimali muhimu kwa taifa na mchango wao haupaswi kusahaulika. Amesema ili kutambua mchango huo, akipatiwa…

Read More

Mfanyabiashara wa mkaa akutwa amefariki dunia pembezoni mwa tanuru

Pangani. Mfanyabiashara wa mkaa, Michael Yohana (43), amekutwa amefariki dunia pembezoni mwa tanuru la mkaa wakati akiendelea na shughuli za kuandaa tanuru hilo kwa ajili ya uzalishaji. Akisimulia tukio hilo wakati wa shughuli za mazishi yaliyofanyika leo, Jumatano Septemba 3, 2025, katika Kijiji cha Langoni wilayani Pangani, mke wa marehemu, Sophia Marandu, amesema tukio hilo…

Read More