Chadema yasisitiza miili ya waathirika wa vurugu za Oktoba 29, izikwe kwa heshima
Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa Chadema, John Heche ameitaka Serikali kuwasilisha na kukabidhi miili ya watu wote waliouawa kabla, wakati na baada ya 29 Oktoba 2025, ili miili hiyo izikwe kwa heshima. Kauli ya kiongozi huyo ni msimamo wa chama hicho kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29,2025 ambapo yalifanyika maandamano yaliyozaa vurugu katika mikoa…