
Mpinzani wa Museveni anayetuhumiwa kwa uhaini agoma kufika mahakamani
Mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye, amegoma kuhudhuria kesi yake ya uhaini akimtuhumu jaji anayesimamia kesi hiyo kuwa na upendeleo. Besigye, aliyewahi kuwa daktari wa Rais Yoweri Museveni na mgombea wa nafasi ya urais mara nne nchini Uganda, anashikiliwa na mamlaka za kiusalama kwa tuhuma za uhaini dhidi ya serikali. Ifahamike kuwa Besigye aliwekwa…