Sungusungu waliohukumiwa kwa mauaji walivyoepa kitanzi
Arusha. Mahakama ya Rufaa imebatilisha hukumu ya kunyongwa hadi kufa iliyokuwa imetolewa dhidi ya sungusungu watatu baada ya kutiwa hatiani kwa mauaji ya mfanyakazi wa Chemi and Cortex Industries Limited, David Albert. Katika rufaa ya jinai namba 503/2024, Juma Said, Emmanuel John na Aman Saniel wameachiwa huru. Awali, Mei 4, 2023, Mahakama Kuu ilikuwa imewahukumu…