Mzee aliyeshtakiwa kwa mauaji ya mwanaye anusurika kitanzi

Arusha. Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, imemuachia huru Ernest Mashurano (71), aliyekuwa ameshtakiwa kwa mauaji ya binti yake, Namala Ernest (13), baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha kesi dhidi yake. Mauaji hayo yalitokea Julai 15, 2024 katika Kijiji cha Kibimba wilayani Kyerwa mkoani Kagera, ambapo mwili wa Namala ulikutwa ukielea juu ya kisima cha…

Read More

Baada ya furaha, abiria waacha vilio Magufuli

Dar es Salaam. Kati ya Novemba 30 hadi Desemba 7, mwaka huu zilikuwa siku za neema kwa wafanyabiashara kwenye stanedi kuu ya mabasi ya Magufuli, jijini Dar es Salaam kutokana na utitiri wa abiria waliokuwa wakisafiri kwenda mikoani. Idadi kubwa ya abiria ilikuwa neema kwa wenye mabasi na wafanyabiashara ndogondogo waliopo ndani na nje ya…

Read More

Dk Mwinyi azitaka taasisi kuacha muhali kukomesha ukatili wa kijinsia

Unguja. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi amezitaka taasisi zinazopinga ukatili wa kijinsia kuacha kuoneana muhali ili kukomesha vitendo hivyo vinavyoendelea nchini. Amesema kuoneana muhali ni miongoni mwa sababu zinazochangia kukosekana kwa haki na utayari wa kupambana na janga hilo linalolitafuna Taifa. Rais Mwinyi alisema hayo leo Jumatatu Desemba 8, 2025  katika hafla maalumu…

Read More

Serikali yaja na mkakati kukomesha uagizaji bidhaa nje

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema Serikali imepanga kuokoa Sh2.8 trilioni kutokana na uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi. Amesema utekelezaji wa hilo utafanyika kwa Serikali kuhakikisha bidhaa nane kati ya 96 zinazoagizwa nje ya nchi zinaanza kuzalishwa nchini kupitia wawekezaji. Hatua hiyo ya…

Read More

JK AENDELEA KUWA KINARA WA ELIMU DUNIANI

Rais Mstaafu Jakaya Dkt. Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia Masuala ya Elimu Duniani (Global Partnership for Education – GPE) ameendelea na jitihada za kukuza elimu duniani. Kwa nafasi yake ya Mwenyekiti wa Bodi ya GPE alisimamia Mkutano wa mwisho wa Bodi hiyo wa kuhitimisha Mpango wa 4…

Read More

Serikali yatoa kauli maandamano ya Desemba 9

Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amesema kilichopangwa kufanyika nchi nzima Desemba 9, 2025 sio maandamano bali ni mapinduzi kwa kuwa  hayapo kisheria. Amesema maandamano hayo yanayodaiwa hayana ukomo kufanyika nchi nzima ni kinyume cha sheria kwa kuwa hakuna ombi lolote la kimaandishi la kufanyika maandamano hayo, hakuna anayeratibu na wala…

Read More