Dar City, Fox Divas watwaa ubingwa wa betPawa NBL 2025

Na Mwandishi wetu Timu ya Dar City kwa upande wa wanaume na Fox Divas kwa upande wa wanawake zimetwaa ubingwa wa mashindano ya klabu bingwa ya mpira wa kikapu Tanzania (betPawa NBL 2025) yaliyomalizika Jumamosi kwenye uwanja wa Chinangali, mkoani Dodoma. Dar City ilitwaa kombe hilo baada ya kuichakaza Kisasa Heroes kwa pointi 80-51 wakati…

Read More

ULEGA AMSIMAMISHA KAZI ‘BOSI’TEMESA

:::::::: SERIKALI kupitia Wizara ya Ujenzi imemsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za uzembe, usimamizi dhaifu na ubadhirifu dhidi yake na viongozi wengine wa taasisi hiyo.  Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ametangaza hatua hiyo jijini Dar es Salaam leo akisema hatua hiyo imefuatia malalamiko ya…

Read More

Bodaboda wataka polisi imwachie diwani mstaafu Chadema

Mbeya. Vijana wa Kata ya Kiwira wilayani Rungwe wamekemea vitendo vya uvunjifu wa amani, huku wakiliomba Jeshi la Polisi kumuachia huru aliyekuwa diwani wa Kata hiyo, Simon Kiraiti (Chadema) na kumpa heshima maalumu ya mtumishi mstaafu. Wakizungumza leo Desemba 7,2025 wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya udereva kwa waendesha pikipiki ‘bodaboda’ wamemshukuru Mbunge wa Mbeya…

Read More

Watumishi legelegewaonywa wilayani hai | Mwananchi

Hai. Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, wametakiwa kuweka mikakati madhubuti na kutilia mkazo suala la ukusanyaji wa mapato, ili kuiwezesha halmashauri kuwaletea wananchi maendeleo yanayoonekana. Wito huo umetolewa leo, Desemba 7, 2025, na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Kiseo Nzowa, katika mkutano wa kwanza wa baraza la madiwani uliofanyika katika…

Read More

Wahitimu wa Furahika wahimiza kufuata maadili katika kazi

NA MWANDISHI WETU WAHITIMU 121 wa Chuo cha Ufundi Stadi, Furahika wametakiwa kuzingatia maadili wanapokwenda kwenye mafunzo kwa vitendo ili kupata fursa ya kupata ajira Mwenyekiti wa Bodi chuo hicho, Suddy Kassim Suddy ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Tabata, ametoa wito huo kwa wahitimu hao wakati wa mahafali Chuo hicho Kilichopo Buguruni Malapa…

Read More

Askofu Malasusa: Udini silaha hatari kwa amani ya Taifa

Dar es Salaam. Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Alex Malasusa amemkemea matamko yenye lengo la kuigawa na kuchochea chuki kwenye jamii dhidi ya dini zao. Akizungumza katika Ibada ya uzinduzi wa jengo la kuabudia KKKT Usharika wa Madale Bethel leo Desemba 7, 2025, Askofu Malasusa amewashukuru Watanzania kwa kuitikia wito…

Read More

Sherehe za harusi zinavyopewa kipaumbele ndoa zikikosa hamasa

Dar es Salaam. Sherehe za harusi zinaendelea kuwa matukio ya kijamii yanayovutia umati na kuonekana kwenye mitandao ya kijamii. Hata hivyo, ibada ya ndoa, ambayo ni kiini cha tukio, imeonekana kuhudhuriwa na watu wachache ikilinganishwa na zamani. Maendeleo ya teknolojia, vipaumbele vipya vya maisha, mizigo ya kiuchumi na mitazamo mipya ya uhusiano vinaibuliwa kama sababu…

Read More

Msigwa: Tunajitosheleza kibajeti | Mwananchi

Dar es Salaam. Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema Tanzania inajimudu kuendesha bajeti kuu ya Serikali bila kutegemea msaada kutoka nje, hata ikitokea msaada huo umekosekana. Msigwa amesema hayo jana, Jumamosi Oktoba 6, 2025, alipozungumzia masuala mbalimbali ya kitaifa katika mahojiano maalumu na kituo cha televisheni cha Star TV. Akizungumzia mjadala wa kujitegemea kufuatia…

Read More