WAZIRI MKUU AWAAGIZA WATENDAJI WA SERIKALI KUANDAA JEDWALI LA UTEKELEZAJI UTATUZI WA KERO ZA WANANCHI
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amewaagiza watendaji wa Serikali kuandaa jedwali la kuonesha namna walivyotatua kero za wananchi katika kila wiki ya mwisho wa mwezi. Amesema hayo leo Jumapili (Machi 01, 2026) katika mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi za Zamani, Babati Mjini mkoani Manyara. Amesema kuwa Serikali haiwezi kukubali utaratibu wa kulimbikiza matatizo ya watu…