MBUNGE MUTASINGWA AWASHAURI WAANDISHI WA HABARI KUIBUA CHANGAMOTO ZA JAMII ILI ZIPATIWE UFUMBUZI
Na Diana Byera,Bukoba Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini mkoani Kagera Mhandisi Johnston Mutasingwa,amewashauri waandishi wa habari wa Manispaa ya Bukoba kuibua habari za uchambuzi zinazouhusu changamoto zinazowakabili wananchi ili zijulikane na kutafutiwa ufumbuzi wa kina. Pia amewaomba watoe ushirikiano kwa viongozi walioko madarakani kisha kuitangaza miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na serikali…