
Umuhimu wa wanandoa kutunza siri
Kuna busara wakati wa kuwafunda wanawali katika jamii moja nchini Uganda isemayo kuwa wanapoolewa lazima wajifunze kufunga miguu na kufungua macho badala ya kufungua miguu na kufunga macho. Hii hufanyika wakati mwali akijiandaa kwenda kwa mumewe. Wazazi hufanya hivyo kwa kujua kuwa nyumbani kwa mwali huacha kuwa kwao na huko aendako ndiko hugeuka kwake. Hamjasikia…