
Hekaya za malevi: Akili mnemba kizibo cha akili – 2
Dar es Salaam. Siwezi kubishana na umati unaodai kuwa akili mnemba ni maendeleo. Hoja yangu ni lugha inayotumika tukisema “Maendeleo ni kutoka mahala na kwenda mahala pengine”, haimaanishi kwenda kinyumenyume ni maendeleo. Hivyo nakusudia kusema kuwa matumizi ya akili mnemba bado hayajaeleweka sawasawa miongoni mwa watumiaji wake. Wanaiweka mbele wakidhani kuwa ina silika za ufundishaji….