Magazeti
NI VYEMA SHERIA YA HUDUMA YA HABARI ZANZIBAR IKAPITISHWA KABLA YA UCHAGUZI MKUU UJAO.
Na Masanja Mabula, PEMBA. BARAZA la Wawakilishi Zanzibar ndio chombo chenye mamlaka ya kutunga na kuzirekebisha sheria ambazo zinaonekana kupitwa na wakati pamoja na zile kandamizi zinazonyima uhuru wa baadhi ya makundi. Zipo sheria ambazo Baraza la Wawakilishi limetunga ambazo zinakwaza uhuru wa Habari na uhuru wa kujieleza kama Kifungu cha 30 kinachompa mamlaka makubwa…
Mume wa Rais mpya wa Namibia asimulia alivyokutana na mke wake Zambia
Windhoek. Ijumaa iliyopita, Rais mteule wa Namibia, Netumbo Nandi-Ndaitwah aliapishwa kuwa Rais wa tano wa Namibia baada ya kushinda uchaguzi wa Novemba 27, 2024 akiwa ni mgombea wa chama tawala cha Swapo. Nandi-Ndaitwah siyo jina geni kwenye siasa za Namibia, wengi wanamfahamu alivyoshiriki harakati za ukombozi wa taifa hilo hadi lilipopata uhuru mwaka 1990 na…
Ndanga, mzee anayetembelea kilomita mbili kila siku kufuata gazeti la Mwananchi
Iringa. Mzee Pascal Ndanga, (90), ambaye ni mkazi wa mtaa wa Kijiweni, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, ameendelea kuwa mfano wa kupenda habari, akitembea kila siku umbali wa kilomita 2 ili kufuata nakala za gazeti la Mwananchi. Kwa miaka mingi, Mzee Ndanga amejiwekea utaratibu wa kufuatilia habari za ndani na nje, akisema anapenda zaidi kusoma…
Manula, Samatta kuwakosa Morocco | Mwanaspoti
KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Hemed Suleiman ‘Morocco’, ametangaza kikosi cha mastaa 24 kitakachoingia kambini kesho Jumamosi, huku nahodha Mbwana Samatta na kipa Aishi Manula wakitemwa kwa sababu tofauti, huku akiwapotezea mastaa watatu wa Singida BS waliobadili uraia. Stars inajiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026…