Buriani, Sheikh Abuu Iddi, mwanazuoni wa aina yake
Alhamisi Januari 30, 2025 itakumbukwa kuwa siku iliyoacha huzuni kwa wanazuoni, masheikh, wanafunzi wa taaluma za dini ya Kiislamu na Waislamu wa Tanzania kwa kuondokewa na Sheikh Mohamed Iddi Mohamed Husein Kisodya Mahede, maarufu kwa jina la Sheikh Abuu Iddi. Huyu alikuwa mwanazuoni maarufu wa Kiislam na Mratibu wa Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa…