Dhamira inayowezekana: kuwapa wateja kipaumbele miaka 25 ijayo
Leo tunapoanza Wiki ya Huduma kwa Wateja ya mwaka 2025 chini ya kauli mbiu “Dhamira: Inawezekana,” najikuta nikitafakari kwa kina maana ya wakati huu kwa Mwananchi Communications Limited (MCL), na kwangu binafsi kama mtu niliyekabidhiwa kuongoza jahazi hili. Hii si Jumatatu ya kawaida. Ni mwanzo wa maadhimisho ya kimataifa ya ubora wa huduma, na pia…