Wananchi kupewa mabomu baridi kukabiliana na tembo Lindi, Ruvuma
Tunduru. Wizara ya Maliasili na Utalii imepeleka askari wanyamapori kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (Tawa) kuwafundisha wananchi wanaoishi katika maeneo yanayozunguka hifadhi na mapori, namna ya kukabiliana na wanyamapori, hasa tembo wanaokatisha kwenye makazi yao. Mafunzo haya yanatolewa katika Wilaya za Tunduru na Namtumbo mkoani Ruvuma na Wilaya ya Liwale mkoani Lindi, yakiwa yanahusisha…